Madaktari bingwa kutoa huduma ya upimaji na matibabu kwa gharama nafuu Kagera

168
0
Share:

Wananchi wa Mkoa wa Kagera na viunga vyake wametangaziwa kujitokeza kwa wingi katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kagera kwa ajili ya kupatiwa huduma za Madaktari bingwa,zoezi linalotarajia kufanyika Septemba 18-24,2017, Hospitalini hapo.

Kwa mujibu wa taarifa yake Mganga Mfawidhi wa hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kagera,  imehimiza Wananchi wote kujitokeza bila kukosa kupatiwa huduma za madaktari hao bingwa kuanzia siku hiyo ya Septemba 18 ambayo itaendelea hadi Septemba 24.

“Madaktari hao bingwa wanatarajia kutoa huduma za upimaji, uchunguzi na matibabu. Hii ni kwa gharama nafuu kabisa ambayo pia ni tofauti na zile zinazochangiwa katika Hospitali kubwa hapa nchini zikiwemo za Bugando, KCMC na Muhimbili.

Miongoni mwa huduma zitakazotolewa ni pamoja na Macho, Pua, Koo, Masikio, Mfumo wa mkojo kwa wanaume, upasuaji, magonjwa ya wanawake, pressure, sukari , moyo, mifupa. Pia kutakuwapo na mabingwa wa mionzi, usingizi, meno, na ngozi.

Kwa bei zitakazokuwa zinatumika ni za chini ikiwemo kumuona Daktari ni sh. 5,000/= Badala ya Sh. 25,000 hadi 30,000 kama wanavyofanya Hospitali kubwa hapa nchini.  Kwa upande wa gharama ya upasuaji wowote itakuwa sh.30,000 badala ya  Laki Nne hadi Milioni moja  kwenye Hospitali zingine hapa nchini” ilifafanua taarifa hiyo.

 

 

Share:

Leave a reply