Mahafali ya nne ya kituo cha Jemolojia kufanya kesho Mei, 19

324
0
Share:
Wahitimu wa awamu ya nne wa mafunzo ya ukataji na uongezaji thamani madini ya vito katika Kituo cha Jemolojia Tanzania  (TGC), wanatarajiwa kufanyiwa mahafali kesho, Mei 19, 2017 jijini Arusha. 
Kamishna wa Madini Tanzania, Mhandisi Benjamin Mchwampaka, amesema kuwa, kuanzishwa kwa Kituo hicho ambacho huendesha mafunzo husika, ni moja ya mafanikio makubwa katika sekta ya madini nchini. 
Akifafanua zaidi, Mhandisi Mchwampaka amesema kuwa, mafunzo hayo kwa sasa hutolewa kwa wanawake watanzania tu ili kuwawezesha kujiinua kiuchumi. 
“Mafunzo hutolewa kwa muda wa miezi sita darasani (nadharia)  na mwezi mmoja wa mafunzo kwa vitendo.”
Aidha, ameeleza kuwa, mafunzo hayo hutolewa bure kwa wahusika kwa ufadhili wa Mfuko maalum unaochangiwa na wafanyabiashara mbalimbali wa madini nchini. 
Kuhusu suala la ajira kwa wahitimu wa mafunzo husika, Kamishna Mchwampaka amesema kuwa Serikali inaangalia uwezekano wa kuwawezesha kwa kuwanunulia vitendea kazi kupitia vikundi vya ujasiriamali watakavyounda ili waweze kujiajiri.
Mahafali hayo ya nne yanatarajiwa kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali, ambapo Mgeni Rasmi atakuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Dk. Mhandisi Juliana Pallangyo.
Jumla ya wanawake 18 kutoka mikoa mbalimbali nchini watatunukiwa vyeti vya kuhitimu mafunzo hayo kesho ambapo watafanya idadI ya wahitimu toka kuanzishwa mafunzo hayo kufikia 65.
Na Veronica Simba
Share:

Leave a reply