Mahakama Kuu kanda ya Dar yatupilia mbali mapingamizi ya Prof. Lipumba

245
0
Share:

Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam imetupilia mbali mapingamizi yaliyowekwa na Mwenyekiti wa Chama cha CUF anayetambuliwa na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, Profesa Ibrahim Lipumba na wenzake, katika kesi ya RITA kuhusu Bodi ya Wadhamini.

Kupitia taarifa yake aliyoitoa mchana huu kwa vyombo vya habari, Naibu Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano kwa Umma CUF, Mbarala Maharagande amesema
Jaji Wilfred Dyansobera anayesimamia kesi hiyo, ameeleza kuwa Mahakama imejiridhisha kwamba mapingamizi yote yaliyowasilishwa na upande wa washitakiwa hayana nguvu za Kisheria.

CUF upande unao muunga mkono Katibu Mkuu wa chama hicho, Maalim Seif Sheriff Hamad kupitia Mbunge wake Ally Salehe ilifungua Shauri la Msingi la Madai (Civil Case No. 13/2017) linalohusu uhalali wa wajumbe wa bodi ya wadhamini ya CUF iliyosajiliwa na RITA dhidi ya Lipumba na wenzake.

Pia ulifungua Shauri la Jinai Na. 50/2017 (Contempt of Court Proceedings) dhidi ya Lipumba na wenzake, linahusiana na kughushi nyaraka kwa lengo la kuingilia na kuharibu mwenendo wa mashauri yaliyopo mahakamani hapo.

Share:

Leave a reply