Mahakama Kuu ya India yapiga marufuku taraka ya maneno

730
0
Share:

Mahakamu Kuu nchini India imepiga marufuku talaka ya Kiislamu ya kutamka neno talaq mara tatu kutumika kuvunja ndoa kwa watu ambao wameoana na kuwa hilo ni kosa kwa mujibu wa sheria ya nchi hiyo.

Uamuzi wa makahakamu kuu ya nchi hiyo umekuja baada ya wanawake watano kufungua kesi katika mahakama hiyo kwa wakati tofauti wakitaka takala ya kutamka neno talaq ifute.

Namna ya utolewaji wa takala hiyo ulikuwa ukiruhusiwa kutolewa kwa njia tofautitofauti ikiwa ni pamoja na kutamka maneno matatu, kutuma ujumbe mfupi wa meseji (SMS), kutuma ujumbe kwa kutumia WhatsApp na hata kutumia Skype.

Awali wakati ikiruhusiwa kutumiwa aina hiyo ya talaka inaelezwa kuwa imewaathiri wanawake wengi nchini India kwa muda mrefu, jambo ambalo lilisababisha kuwepo na idadi kubwa ya wanawake ambao wanaachika.

 

Share:

Leave a reply