Majaliwa afungua Mkutano wa ALAT

250
0
Share:

Waziri Mkuu wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa amekuwa mgeni rasmi katika mkutano maalum wa uchaguzi wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa (ALAT), umeofanyika mkoani Dodoma.

IMGS0592

Waziri mkuu, Kassim Majaliwa akimsikiliza Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TANTRADE, Edwin  Rutageruka wakati alipotembelea banda la maonyesho  la TANTRADE kabla ya kufungua Mkutano Mkuu Maalum wa Uchaguzi wa Jumuiya ya Tawala  za Mitaa (ALAT),Dodoma. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

IMGS0610

Wasanii wa kikundi cha Nyota cha Dodoma  wakitumbuiza katika Mkutano Mkuu Maalumu wa Jumuiya ya Tawala za Mikoa kwenye Kituo cha Mikutano cha Dodoma 

IMGS0621

Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Suleiman Jafo kizungumza kabla ya kumakaribisha Waziri Mkuu, Kasim Majaliwa kufungua Mkutano Maalum wa Uchaguzi wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa kwenye Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Dodoma

IMGS0627

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza wakati alipofungua mkutano Mkuu Maalum wa Uchaguzi wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania  (ALAT) kwenye  Kituo cha Mikutano cha Dodoma

IMGS0632

IMGS0720

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi Mwenyekiti wa Jumuiya ya Tawala za Mikoa (ALAT), Gulam Mkadam Taarifa ya Utafiti  kuhusu Sekta ya Umma na Binafsi kwenye serikali za Mitaa wakati alipoizindua baada ya kufungua Mkutano Mkuu Maalum wa uchaguzi wa Jumuiya ya Tawla za Mitaa Tanzania (ALAT). Kulia ni Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawla za Mikoa na Serikali za Mitaa, Suleiman Jafo.

IMGS0635

Baadhi ya washiriki wa Mkutano Mkuu Maalum wa Uchaguzi wa  Jumuiya ya Tawala za Mikoa (ALAT) wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kasim Majaliwa wakati alipofungua Mkutano huo

Share:

Leave a reply