Majibu ya Fabregas baada ya kuenea tetesi za kuambiwa atafute timu nyingine

272
0
Share:

Jumapili ya Agosti, 28 mitandao mbalimbali ya habari iliripoti habari ya kuwa kiungo wa Chelsea, Cesc Fabregas amepewa makavu na kocha wa klabu hiyo, Antonio Conte akimtaka atafute klabu ya kwenda kutokana na kutokuwa na nafasi katika kikosi hicho.

Taarifa hiyo ilieleza kuwa, Conte amemwambia Fabregas maneno hayo kutokana na kutoridhishwa na uwezo wa kiungo huyo aliyejiunga Chelsea mwaka 2014 akitokea Barcelona na hivyo nafasi yake kuchukuliwa na wachezaji wengine.

Kupitia akaunti yake ya Twitter, Fabregas amekanusha taarifa hiyo kuwa siyo kweli na kwa sasa kocha huyo anaangalia uwezo wake hivyo ataendelea kuitumikia klabu hiyo na kuhakikisha ikipata ushindi katika michezo yake.

“Kinyume na kilichoandikwa ni kuwa nina mahusiano mazuri na meneja na hajawahi kuniambia kuwa ninaweza kuondoka,

“Nitaendelea kupigana kwa ajili ya klabu mpaka mwisho wangu, nitaonyesha uwezo wangu wote. Nitawajibika kwa ajili ya Chelsea na malengo yangu ni kuisaidia kupata ushindi katika michezo yake,” aliandika Fabregas.

Share:

Leave a reply