Majibu ya Griezmann kuhusu kuhusishwa kujiunga Arsenal

991
0
Share:

Winga wa Atletico Madrid, Antoine Griezmann amevunja ukimya kuhusu tetesi za kuwa anaweza kujiunga na Arsenal baada ya mchezaji mwenzake wa timu ya taifa ya Ufaransa, Laurent Koscielny kumshawishi kujiunga na washika bunduki wa London.

Griezmann alisema anafahamu kuwa Arsenal ni timu nzuri na anavutiwa na uchezaji wake lakini hawezi kujiunga kwa sasa kwani bado anataka kusalia Atletico Madrid kwa muda mrefu zaidi.

“Alizungumza na mimi kuhusu Arsenal lakini Madrid ni pazuri kwangu. Sihitaji kuondoka, nina furaha kuwa hapa,” alisema Griezmann ambaye pia amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa Ufaransa 2016 na kuongeza kuwa.

“Nina furaha na nitaendelea kusalia hapa lakini Arsenal ni timu nzuri na wanacheza mpira vizuri.”

Griezmann ambaye ana miaka 25 alijiunga Atletico Madrid mwaka 2014 akitokea Real Sociedad na tangu alipojiunga na klabu hiyo amekuwa akizivutia klabu nyingi kubwa barani Ulaya kutokana na kuonyesha kiwango bora.

Share:

Leave a reply