Majibu ya Msemaji wa Bunge baada ya Viongozi Kamati ya Viwanda kuachia ngazi

3102
0
Share:

Msemaji wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Bwana Owen Mwandumbya (Pichani juu)  amesema kuwa ofisi ya Bunge imepokea barua ya kujiuzulu kwa viongozi wa Kamati ya Viwanda na Biashara kwa nafasi ya Mwenyekiti wa kamati ya viwanda na biashara, Dk Dalali Kafumu na makamu wa kamati hiyo Vick Kamata, mapema leo kufuatia barua yao hiyo ya kujiuzulu.

Bwana Owen akizungumza kwa njia ya simu ya MO Blog, amebainisha kuwa, tayari ofisi ya Bunge imepokea barua yao hiyo na kueleza kuwa, Wajumbe wa Kamati hiyo wanayo nafasi ya kuchagua viongozi wapya.

“Barua ya viongozi wa Kamati kujiuzulu tumeipata. Kwa suala la kuziba nafasi lipo kwa wajumbe wenyewe wa Kamati ambao wataweza kuchaguana na kisha kutoa taarifa kwa Spika” alifafanua msemaji wa Bunge wakati wa kujibu swali la MO blog lililotaka kujua hatua zipi zitafuata.

Mapema leo Machi 20.2017, Viongozi hao wa Kamati ya  viwanda na biashara waliandika barua yao ya kijiuzulu nafasi zao  kwa maelezo kuwa Serikali inaingilia majukumu yao katika utendaji kazi na hivyo hawaoni sababu za kuendelea huku wakikabidhi barua yao hiyo  ya kujihuzuru ofisi ya spika.

Aliyekuwa Mwenyekiti wa kamati ya viwanda na biashara, Dk Dalali Kafumu aliyejiuzulu kamati hiyo

Aliyekuwa Makamu wa kamati hiyo ya Viwanda na Biashara, Mh. Vick Kamata

Msemaji wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Bwana Owen Mwandumbya.

Barua ya kujiuzulu nafasi hizo

Share:

Leave a reply