Majimaji yatuma salamu Msimbazi

251
0
Share:

Timu ya Majimaji imetamba kuifunga timu ya Simba Sc katika mchezo wa VPL inayotarajiwa kuchezwa Jumamosi hii katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Mjumbe wa Kamati ya Utendaji Majimaji, Salumu Masamaki amesema timu hiyo imeshawasili Dar es Salaam na inafanya mazoezi ya kutosha ili kuwakabili wekundu wa msimbazi Simba.

“Maandalizi ya mechi ya Jumamosi yako vizuri, Majimaji iko vizuri, timu imeshawasili tumefanya mazoezi ya nguvu na ninawahakikishia tutafanya mauaji ya kutisha lazima turudi na pointi tatu songea,” amesema.

Masamaki amesema baada ya kampuni ya Symbion iliyokuwa inaidhamini timu hiyo kumaliza mkataba wake, imepata mdhamini mpya Kampuni ya GSM.

“Kuhusu udhamini ni kweli GSM inatudhamini baada ya mkataba wa symbion kuisha na muda wowote kuanzia sasa mkataba utasainiwa. GSM wako kwenye timu wanaihudumia. Hivi sasa Ukata wa pesa majimaji mwisho,”

Masamaki amewahakikishia mashabiki wa Majimaji kuwa timu hiyo haitashuka daraja na itaendelea kufanya vizuri.

“Hatutashuka daraja msimu huu , watu wengi walitabiri kuwa tutashuka daraja msimu uliopita lakini harukushuka, hivyo kwa msimu huu watasubiri sana,” amesema.

Share:

Leave a reply