Makamu wa Rais awapelekea neema ya maji wananchi 7,500 Zanzibar

162
0
Share:

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amesema mtu yeyote anayehakikisha wananchi wanapata maji safi na salama basi anapato lake kwa Mwenyezi Mungu.

Makamu wa Rais ameyasema hayo wakati wa kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa tanki la maji safi na salama lenye uwezo wa kubeba lita laki mbili na nusu (lita 250,000) lililopo Kikwajuni kwa Mselem ambapo watu elfu saba na mia tano (watu 7,500) watanufaika.

Makamu wa Rais amewataka wananchi hao kuwa na Kamati ya Maji mara baada ya mradi huo kukamilika na kuwataka wananchi hao kuchangia huduma ya maji ili waweze kuendesha mradi huo.

Wakati huo huo Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amewataka wazazi wenye watoto wenye ulemavu wawapeleke watoto wao kwenye vituo vitakavyoweza kuwafundisha mambo mbali mbali badala ya kuwafungia ndani.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan akipata maelezo ya ujenzi wa miundo mbinu katika mradi wa maji utakao nufaisha wakazi wa elfu saba mia tano (7500) katika Shehia 4 mara baada ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa tanki la maji safi Kikawajuni kwa Mselem katika jimbo la Kikwajuni, wengine pichani ni Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni Mhandisi Hamad Masauni na Mkuu wa mkoa wa mjini Magharibi Ndugu Ayoub Mohammed Mahmoud . (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

Makamu wa Rais amesema walemavu wamejialiwa vipaji na uwezo wa hali ya juu kama wataendelezwa.

Makamu wa Rais ameyasema hayo wakati wa hafla ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa Jengo la watu wenye ulemavu Shauri Moyo, Mikunguni.

Makamu wa Rais ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa yupo kwenye ziara ya kuhamasisha shughuli za maendeleo na kukagua miradi ya Chama Cha Mapinduzi Unguja, Zanzibar.

Share:

Leave a reply