Makamu wa Rais Samia awatembelea majeruhi Hospitali ya Mt. Meru, Arusha

633
0
Share:

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amewatembelea majeruhi wa basi la shule ya Lucky Vincent waliopata ajali ambayo ilisababisha vifo vya wanafunzi  32 na wawili pamoja na dereva mmoja.

Makamu wa Rais aliongozana na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo na viongozi wengine wa mkoa ambapo aliweza kuwajulia hali majeruhi hao waliolazwa kwenye hospitali mkoa wa  wa Arusha ya Mt. Meru,  huku baadhi yao wakiendelea kuuguza majeraha.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimjulia hali  Godfrey Tarimo mwenye umri wa miaka 11 ambaye ni mmoja wa majeruhi waliolazwa kwenye hospitali mkoa wa  wa Arusha ya Mt. Meru, Godfrey ni mmoja ya waliojeruhiwa katika ajali waliopata wanafunzi wa Lucky Vincent 

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimjulia hali  Doreen Mshana mwenye umri wa miaka 13ambaye ni mmoja wa majeruhi waliolazwa kwenye hospitali mkoa wa  wa Arusha ya Mt. Meru, Doreen ni mmoja ya waliojeruhiwa katika ajali waliopata wanafunzi wa Lucky Vincent

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimjulia hali  Sadia Isamel Awadhi mwenye umri wa miaka 11 ambaye ni mmoja wa majeruhi waliolazwa kwenye hospitali mkoa wa  wa Arusha ya Mt. Meru, Sadia ni mmoja ya waliojeruhiwa katika ajali waliopata wanafunzi wa Lucky Vincent.

Picha na Ofisi ya Maku wa Rais.

 

 

Share:

Leave a reply