Makatibu Wakuu watembelea kituo mahiri cha kutunza kumbukumbu, Kijitonyama

266
0
Share:

Dkt. Maria Sasabo

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano anayeshughulikia sekta ya Mawasiliano Dkt. Maria Sasabo akitoa maelezo ya kituo mahiri cha kutunza kumbukumbu (Internet Data Centre) kwa Makatibu Wakuu hawapo pichani walipotembelea kituo hicho kilichopo eneo la Kijitonyama Dar Es Salaam.

Katibu Mkuu wa Wizara  ya  Ardhi Dkt. Yamungu Kayandabila (katikati

Katibu Mkuu wa Wizara  ya  Ardhi Dkt. Yamungu Kayandabila (katikati) akitoa maoni  yake kuhusu  kituo mahiri cha kutunza kumbukumbu “ internet Data Centre”,  (wa kwanza kulia) ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya nje na Afrika Mashariki Balozi Ramadhani Mwinyi na (wa kwanza kushoto) ni Kaimu Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango Bibi Florence Mwanri walipokitembelea kituo hicho eneo la Kijitonyama jijini Dar.

Afisa kutoka Kampuni ya Simu Tanzania TTCL Bw. Suleimani Kagobe

Afisa kutoka Kampuni ya Simu Tanzania TTCL Bw. Suleimani Kagobe akitoa maelezo kwa Makatibu Wakuu jinsi mfumo wa umeme unavyofanya kazi walipotembelea katika kituo mahiri cha kutunza kumbukumbu kilichopo eneo la Kijitonyama DSM.(Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano).

Share:

Leave a reply