Makonda awashangaa abiria wa mabasi ya haraka kugoma kushuka vituoni (Audio)

228
0
Share:

Mkuu wa Mkoa wa Dar res Salaam, Paul Makonda amefanya ziara kuangalia utendaji kazi wa magari ya mwendo kasi ambayo yalianza kasi jana Jumanne na kuelezea maoni yake kwa siku moja ambayo magari hayo yameanza kufanya kazi.

Makonda amesema ameshangaa kuona baadhi ya wananchi ambao wanapanda magari hayo wanagoma kushuka pindi wanapofika kituo cha mwisho.

DSC_1903

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Bi. Sophia Mjema wakati alipotembelea kituo cha mabasi yaendayo haraka kilichopo Kariakoo.

“Wapo watu wanapanda gari na hawataki kushuka anapanda asubuhi Kimara yeye anazunguka tu na mimi nimeshangaa kwa mara ya kwanza watu hawa hawapati hata njaa wala maji yeye anazunguka tu … ukishapanda mara moja shuka wengine wapande wajifunze,” alisema Makonda.

Aidha Makonda amewataka wananchi ambao bado wanatumia barabara za mabasi hayo waache mara moja na tayari kuna askari ambao watakuwa wanasimamia barabara hizo ili kuhakikisha mbasi hayo pekee ndiyo yanatumia barabara hiyo.

“Pikipiki, bajaji, hakuna basi wala gari la mtu binafsi naomba wananchi waelewe tutakuwa na askari zaidi ya 43 kulinda hizo barabara,” aliongeza Makonda.

Zaidi unaweza kumsikiliza hapa chini.

DSC_1916

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa DART, Injinia Ronald Lwakatare akizungumza jambo na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda wakati alipokuwa ndani ya basi liendalo haraka ili kuona jinsi linavyofanya kazi. 

DSC_1914

Share:

Leave a reply