Mambo makuu muhimu kutoka kwa Mh.Mrema alipokutana na Wahanga wa Madawa ya Kulevya Dar

329
0
Share:

Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Parole, Mh. Augustino Lyatonga Mrema amekutana na Wahanga wa matumizi wa Madawa ya Kulelvya kwa Mkoa wa Dar es Salaam kwa lengo la kufahamu na kujua changamoto zao wanazokumbana nazo huko mitaani licha ya kuacha matumizi hayo.

Mh. Mrema amekutana na Wahanga hao Jijini Dar es Salaam ambapo amewaambia kuwa kero na maoi yao ameyapokea na atayafikisha kwa Mtukufu Rais ilikuweza kuyafanyia kazi kwa ukaribu.

“Nimepokea kero zenu. Naomba nitaziwakilisha kwa Rais. Kwani ni lazima tutatue tatizo hasa mizizi na hatuwezi kukamata vidagaa na kuacha Mapapa ya madawa ya kulevya yakielea.” Amesema Mrema huku akishangiliwa na Vijana hao.

Mrema amesema kuwa, Mkoa wa Dar es Salaam una wahanga zaidi ya 3,000 ambao wanatumia madawa hayo ya kulevya ambapo suala hilo ni janga kubwa sana na anatarajia kulichaukulia hatua.

Nukuu muhimu za Mh. Mrema alizosema leo:

(1)”Mapapa makubwa wa Madawa ya Kulevya wanajulikana, Wakamatwe mara moja wawekwe ndani na sio vidagaa ambao wanaenda kujaza magereza yetu”

(2)”Wahanga wa madawa ya kulevya wasikamatwe. Wawekewe usaidizi ikiwemo kupelekwa kwenye vituo vyao vya kupatiwa elimu ya jinsi ya kuacha. ikiwemo Mwananyamala, Muhimbili na Temeke.”

(3) Watu 3,000 wanaotumia madawa ya kulevya kwa mkoa wa Dar es Salaam ni janga”

(4) “Watu wanaokamatwa kwa kete moja ama mbili za madawa ya kulevya ndio wanaojaa magerezani”.

(5) “Watu wanaokamatwa na kete wasipelekwe maabusu, bali wapelekwe kwenye vituo na sehemu za kupatiwa madawa ili waache”.

(6)”Wasambazaji na wanaoingiza madawa nchini hawakamatwi, ila watumiaji ndio wanakamatwa?, Nawaombeni Polisi, huo mchezo munaocheza kuwakamata watu hao gerezani sio mahala pao”.

Na Hashim Ibrahim-UDSM-SJMC

DSC_5348

Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Parole, Mh. Augustino Lyatonga Mrema ambaye alikuwa mgeni rasmi akiingia kwenye eneo la mkutano ulioandaliwa kwa ajili ya kukutana na Vijana Wahanga wa Madawa ya kulevya wa Mkoa wa Dar es Salaam.

DSC_5361Baadhi ya Vijana  Wahanga wa Madawa ya Kulevya Mkoa wa Dar es Salaam wakiomba dua wakati wa mkutano huo 

DSC_5372Mwanadada Bi. Teddy Killa akifungua mkutano huo

DSC_5431Mmoja wa wadau wanaopambana na madawa ya kulevya akitoa ushuhuda wake

DSC_5460 DSC_5367 DSC_5448

Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Parole, Mh. Augustino Lyatonga Mrema akiongea na Wahanga hao wa Madawa ya kulevya (Hawapo pichani) wakati wa mkutano huo

DSC_5457

Baadhi ya vijana hao wakishangilia baada ya Mh. Mrema kutoa agizo kwa wanaokamatwa na kete moja ama mbili za dawa za kulevya wasikamatwe na baadala yake wapelekwe kwenye vituo ikiwemo Soba House kupatiwa elimu

DSC_5476

Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Parole, Mh. Augustino Lyatonga Mrema akijadiliana jambo na vijana hao mara baada ya kumaliza mkutano huo

DSC_5478 DSC_5484Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Parole, Mh. Augustino Lyatonga Mrema akipata picha ya pamoja na baadhi ya vijana hao. (Picha zote na Andrew Chale).

Share:

Leave a reply