Mambo mawili ya kufahamu aliyofanya Rais John Magufuli Agosti 23

494
0
Share:

Rais Dk. John Pombe Magufuli amemteua Luteni Kanali Frederick Felix Milanzi kuwa Kamishna wa Operesheni wa Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya akichukua nafasi ya Mihayo Msikela ambaye amerejeshwa Makao Makuu ya Jeshi la Polisi.

Pia Rais Magufuli amezungumza na Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya, Rogers Siyanga ambaye amemhakikishia kuwa kazi ya kukabiliana na tatizo la biashara na manunuzi ya dawa za kulevya inaendelea vizuri na dawa za kulevya ambazo mamlaka inapambana nazo ni bangi, heroine, cocaine, kemikali bashirifu na sasa imeanza kukamata na kuharibu mashamba ya bangi na bangi iliyovunwa.

Share:

Leave a reply