Mambo mawili ya kufahamu kuhusu Ibrahimovic na Mkhitaryan

388
0
Share:

Ukitaja kikosi cha Manchester United kwa msimu wa 2016/2017 huwezi
kuacha kumtaja Zlatan Ibrahimov na Henrikh Mkhitaryan kutokana na umuhimu wao
katika kikosi kinachoongozwa na Jose Mourinho.
Wachezaji wote hao Mourinho aliwatumia katika mchezo wa jana
wa Kombe la Vilabu Barani Ulaya ambapo Man United walikuwa wakipambana na
Anderlecht mchezo ulimalizika kwa sare ya goli moja kwa moja.
Kwa Mkhitaryan pekee katika michezo minne iliyopita ya
Europa League ambayo ameichezea Man United amefunga magoli manne ambayo ni namba
sawa na idadi ya michezo amecheza.
Kwa upande wa Ibrahimovic katika Europa League mpaka sasa
ameshahusika katika magoli nane ambayo Man United wamefunga, amefunga magoli
matano na kutoa pasi za magoli matatu.
Share:

Leave a reply