Mambo mawili ya kufahamu kuhusu Man City na Guardiola katika UCL

518
0
Share:

Michezo miwili ya Ligi ya Mabingwa Ulaya imepigwa usiku wa kuamkia alhamisi ya Machi, 16 ambapo Monaco ilikuwa mwenyeji wa Man City na Atletico Madrid ikiwa mwenyeji wa Bayer Leverkusen.

Mchezo wa Monaco na Man City ulimalizika kwa Monaco kuibuka na ushindi wa goli 3-1, ushindi ambao umefanya magoli ya kufungana kulinganisha na mchezo wa kwanza kuwa ni 6-6 na hivyo Monaco kufuzu kwa goli la ugegeni.

Ushindi wa Monaco licha ya maumivu ya Man City ya kutolewa katika Ligi ya Mabingwa Ulaya pia Man City imekuwa timu ya kwanza katika Ligi ya Mabingwa Ulaya kutolewa katika hatua ya mtoano ikiwa katika mchezo wa kwanza ilifunga magoli matano.

Licha ya hilo pia kocha wake, Pep Guardiola imekuwa ni mara ya kwanza kwake kutolewa katika hatua ya mtoano tangu aanze kufundisha soka katika timu zilizopita ya Barcelona ya Hispania na Bayern Munich ya Ujerumani.

Kocha wa Manchester City, Pep Guardiola.

Matokeo ya mchezo mwingine wa Atletico Madrid na Bayer Leverkusen ni sare ya bila kufungana na hivyo Atletico kufuzu kwa ushindi wa goli 4-2, ushindi ambao iliupata katika mchezo wa kwanza uliopigwa katika dimba la BayArena.

Share:

Leave a reply