Man United yakodi hoteli ya kifahari kwa ajili ya msimu wa 2016/2017

224
0
Share:

Kuna msemo umekuwa ukisema kuwa Tumia Pesa Ikuzoee, hilo limeonekana pia kutokea kwa Manchester United ambayo mwanzoni kwa wiki hii ilitajwa kuwa katika orodha ya timu ya tano za michezo ambazo zinaongoza kwa utajiri duniani.

Katika kujiandaa na msimu wa 201/2017, Manchester United imekodi hoteli ya kifahari ya The Lowry iliyopo katika jiji la Manchester United nchini Uingereza ambayo itakuwa inatumika kwa wachezaji kupumzika wakati wakijiandaa na michezo ya nyumbani.

Inasemekana kuwa Man United wamekodi vyumba zaidi ya kumi kwa msimu mzima ili wanapokuwa na michezo ya nyumbani katika uwanja wake wa Old Trafford waweze kufanya kambi na kuishi katika hoteli hiyo.

Hoteli hiyo ya The Lowry iliyo na hadhi ya nyota tano imekuwa maarufu kwa watu mbalimbali maarufu kupumzika katika hoteli hiyo akiwepo marehemu Muhammad Ali, Adele, Pharrell Williams, Bono, Cristiano Ronaldo na Lady Gaga.

360984B900000578-3687877-image-a-30_1468519139210

3609B85D00000578-3687877-image-a-23_1468517636189

3609B03C00000578-3687877-image-a-16_1468517400136

36097AF900000578-3687877-image-a-14_1468542332570

Cristiano Ronaldo akiwa katika hoteli ya The Lowry.

Share:

Leave a reply