Man United yamalizana na Pogba, sasa yasubiriwa Juventus kuthibitisha

216
0
Share:

Kwa hakika inaonekana kuwa Manchester United imepania kumrudisha mchezaji wake wa zamani, Paul Pogba baada ya taarifa kutoka kuwa tayari Manchester United imefikia makubaliano ya mshahara ya Pogba.

Taarifa hizo zinaeleza kuwa Pogba amefikia makubaliano na Manchester United ya kulipwa Pauni 200,000 kwa wiki baada ya kuwa imekatwa kodi ikiwa ni tofauti ya Pauni 170,000 anayochukua kwa sasa Juventus ya Pauni 30,000.

Jumanne ya Julai, 19 zilitoka taarifa kuwa Manchester United imetuma ofa ya Pauni Milioni 104 kwa Juventus ili kumruhusu Pogba kujiunga na Man United baada ya awali kukataa ofa ya Pauni Milioni 88.

Pia pamoja na hayo inaelezwa kuwa tayari Pogba ameiambia Juventus kuwa anahitaji kuondoka katika klabu hiyo na kujiunga na Manchester United, sehemu ambayo ilimkuza kisoka na kuwa klabu hiyo ni sawa na nyumbani kwake.

Share:

Leave a reply