Man United yamtengea kinda wa Monaco Euro milioni 95

637
0
Share:

Klabu ya Manchester United ya Uingereza imeripotiwa kutenga kitika cha fedha cha Euro milioni 95 ambazo ni sawa na bilioni 229 za Kitanzania kwa ajili ya kupata saini ya mshambuliaji wa Monaco, Kylian Mbappe.

Hatua ya Man United kutaka kumsajili kinda huyo imekuja baada ya Mbappe kuonyesha kiwango kikubwa katika michezo mbalimbali ambayo anayoichezea Monaco ambapo mpaka sasa ameshaifungua magoli 19 kwa msimu wa 2016/2017.

Awali iliripotiwa Man United ilikuwa imetenga milioni 69 lakini pesa hiyo ilionekana kutokukubalika kwa Monaco na hivyo kuongeza dau ambalo limefikia Euro milioni 95.

Man United wapo katika ushindani wa kupata saini ya Mbappe kwani hata Real Madrid nao wanaripotiwa kumfatilia mshamuliaji huyo ili ajiunge na wababe hao kutokea Hispania.

Share:

Leave a reply