Maneno ya Haji Manara kuhusu penati ya Msuva

3814
0
Share:

Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa Simba, Haji Manara ameamua kufunguka kilicho moyoni mwake baada ya kuona baadhi ya mashabiki wa watani zao Yanga wakimsema mshambuliaji wao Simon Msuva.

Manara amefunguka kwa kumtetea Msuva baada ya kukosa penati katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kati ya Mtibwa Sugar na Yanga, mchezo uliopigwa katika uwanja wa Jamhuri, Morogoro na kumalizika kwa sare ya bila kufungana.

Msemaji huyo wa Simba ameandika katika akaunti yake ya Instagram kwa kusema, “Acheni kumsumbua Simon, penalty anakosa Messi!! Kama vp c mmuache?? nyie wa wapi…[email protected]

Acheni kumsumbua Simon, penalty anakosa Messi!! Kama vp c mmuache?? nyie wa wapi…[email protected]

A post shared by Haji S Manara (@hajismanara) on

Share:

Leave a reply