Marekani yaishutumu Korea Kaskazini kulazimisha vita

752
0
Share:

Marekani imeshutumu Korea Kaskazini kuwa inalazimisha kutokea vita kutokana na majaribio ya makombora yake ambayo imekuwa ikiyafanya mara kwa mara ikiwepo la hivi karibuni la nyuklia.

Hayo yamesemwa na Balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa, Nikki Haley ambaye amesisitiza pamoja na majaribio ambayo Korea Kaskazini inayafanya lakini haina mpango wa vita na nchi yoyote.

“Vita sio jambo ambalo Marekani inalihitaji, hatuhitaji jambo hilo litokee sasa lakini nuvumilivu wa chi yetu sio kikomo,” alisema Haley.

Aidha imeripotiwa kuwa Marekani imepanga kuiwekea Korea Kaskazini vikwazo vipya ambavyo vitakuwa na nguvu zaidi ya vilivyopo sasa.

Share:

Leave a reply