Marekani yajitoa mgogoro wa Palestina na Israel

131
0
Share:

Marekani yajitoa katika mazungumzo ya utafutaji wa suluhu ya mgogoro unaokabili mataifa mawili ya Palestina na Israel kuhusu mmiliki halali wa mji wa Yerusalemu.

Rais wa Marekani, Donald Trump aliwaambia waandishi wa habari kwamba serikali yake haina tena cha kuzungumza zaidi juu ya mgogoro huo.

Alisema suala la Yerusalem limetoka kwenye meza ya mazungumzo baada ya uamuzi wake wa kutangaza mji huo kama mji mkuu wa Israel na kuhamisha ubalozi Marekani kutoka mji wa Tel Aviv.

Uamuzi wa Trump juu ya kuutambua Yerusalemu kama mji mkuu wa Israeli ulivunja sera ya miaka mingi ya Taifa hilo ya kutoutambua mji huo kama mji mkuu wa Israel.

Share:

Leave a reply