Marekani yamtaka Odinga kusitisha mpango wa kuapishwa kuwa Rais

331
0
Share:

Nchi ya Marekani imemtaka Kiongozi Mkuu wa Upinzani nchini Kenya Raila Odinga kuacha mpango wake wa kuapishwa kama rais wa nchi hiyo wiki ijayo Desemba 12, 2017. 

Msaidizi wa Katibu wa Masuala ya Afrika Marekani, Donald Yamamoto alipotembelea Kenya,  ametaka kuwepo majadiliano ya pande zote mbili baina ya upinzani na serikali iliyoko madarakani.

Licha ya wito huo, baadhi ya viongozi wa serikali wameonya kwamba tukio hilo la kuapishwa Odinga, linaweza kuhusishwa na kosa la uhaini. 

Odinga baada ya uchaguzi Mkuu wa Kenya kufanyika alitoa malalamiko kuhusu mapungufu yaliyojitokeza kwenye uchaguzi huo na kupelekea uchaguzi kurudiwa ambapo Uhuru Kenyata alishinda kwa kishindo.

Chanzo: BBC

Share:

Leave a reply