Marekani yaonywa kutotangaza Jerusalem kuwa mji mkuu wa Israel

557
0
Share:

Nchi ya Jordan imeionya Marekani kutoutangaza mji wa Jerusalemu kuwa mji mkuu wa Israeli kwa kuwa hatua hiyo inaweza kuzua ghadhabu kubwa kwa nchi za kiarabu na ulimwengu wa Kiislamu.

Waziri wa Mashauri ya Nchi za Kigeni nchini Jordani, Ayman Safadi alizungumza na Waziri wa Mashauri wa Nchi za Kigeni wa Marekan,i Rex Tillerson kuhusu hatua hiyo na namna itakavyoleta hatari.

Onyo hilo limekuja baada ya uwepo wa uvumi kwamba Rais wa Marekani Donald Trump hivi karibuni anatarajiwa kutangaza suala hilo ili kutimiza ahadi yake aliyoitoa wakati wa kampeni za uchaguzi, hata hivyo Mkwe wa Trump, Jared Kushner amesema bado hakuna uamuzi wowote uliofanywa kuhusu suala hilo.

Kwa upande wake Rais wa Palestina Mahmoud Abbas anajaribu kupata msaada kutoka kwa mataifa wa kumshawishi Trump kutoutangaza Mji wa Jerusalemu kuwa mji mkuu wa Israel, ambapo ofisi yake iliwapigia simu viongozi wa dunia akiwemo rais wa Ufaransa Emanuel Macron na rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogarn.  

Share:

Leave a reply