Marekani yataka Korea Kaskazini iwekewe vikwazo

519
0
Share:

Marekani yataka mataifa kuitenga Korea Kaskazini ili kuishinikiza kuacha matumizi ya silaha za nyuklia.

Makamu wa Rais wa Marekani, Mike Pence amesema nchi hiyo ina amini kuwa njia yenye mafanikio ili kuishinikiza Korea Kaskazini kuachana na mpango wake wa kutumia silaha za nyuklia ni mazungumzo ya kimataifa kuishinikiza na kuitenga nchi hiyo kutokana na msimamo wake,lakini amesisitiza kuwa njia zote zina uzito wake.

Pence ameyasema hayo wakati akizungumza na Naibu Waziri mkuu wa Japan Taro Aso, mjini Tokyo ambapo wamekubaliana kuweka msukumo wa Kidiplomasia na kiuchumi dhidi ya Korea Kaskazini ili kuishinikiza kuachana na mpango wake wa silaha za nyuklia.

Amesema Marekani itaendelea kushirikiana na Japan na washirika wengine katika ukanda na China, kuweka vikwazo vya kidiplomasia na kiuchumi dhidi ya Korea Kaskazini ili iachane na mpango wake wa silaha za nyuklia. Hata hivyo, amesema mapendekezo yote yanaendelea kujadiliwa.

Share:

Leave a reply