Marekani yazuia dola milioni 65 kwa Wapalestina

212
0
Share:

Marekani imezuia fedha kiasi cha dola milioni 65 zilizopangwa kwa ajili ya kulisaidia Shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia wakimbizi wa Palestina (UNRWA). 

Maafisa wa Wizara ya Mambo ya Nje Marekani jana walisema nchi hiyo itatoa dola 60 kati ya 125 zilizopangwa kwenda UNRWA, huku ikisisitiza kuwa uamuzi huo hauna lengo la kuwashinikiza viongozi wa Palestina, kufuatia hatua ya Rais Donald Trump kutishia kutoa msaada kwa wapalestina. 

Msemaji wa Wizara hiyo, Heather Nauert amesema hatua hiyo haikusudii kumuadhibu mtu yeyote na kwamba serikali ya Marekani inapenda kuona nchi nyingine hasa zinazoikosoa nchi hiyo kutokana na msimamo wake dhidi ya Wapalestina kujitokeza kulisaidia shirika la UNRWA. 

Hata hivyo, Mkurugezi wa UNRWA, Pierre Krahenbuhl  amesema ameshhitushwa na uamuzi wa Marekani na kuzitaka nchi wanachama wa UN kulichangia shirika hilo.

Share:

Leave a reply