Maria Sharapova afungiwa miaka miwili kucheza tenesi, Nike watoa msimamo wao

196
0
Share:

Baada ya mwezi Januari mcheza wa tenesi, Maria Sharapova vipimo kuonyesha kuwa anatumia dawa za kuongeza nguvu mwilini, hatimaye hukumu yake imetolewa na Shirikisho la Kimataifa la Tenesi kwa kumfungua miaka miwili asicheze tenesi.

Sharapova aligundulika kutumia madawa hayo wakati alipofanyiwa vipo katika mashindano ya Australia Open na baada ya kugundulika kutumia dawa hizo alizuiliwa kushiriki mashindano hayo na kusubiri hatua ambazo zingekufuatia ambapo sasa ndiyo hukumu imetolewa.

Hata hivyo taarifa zinaeleza kuwa Sharapova amepanga kwenda katika mahakama ya michezo kwa ajili ya kukata rufaa ya adhabu hiyo ambayo imetolewa kwake kwa kutumia madawa ya kuongeza nguvu  ya meldonium.

Wakati hayo yakimkuta, kampuni ya vifaa vya michezo ya Nike ambayo inafanya kazi na Sharapova imetoa taarifa kuwa itaendelea kufanya kazi na Sharapova na wanaamini ataenda mahakamani kukata rufaa ili arejee michezoni.

Share:

Leave a reply