Martha Mlata achaguliwa kuwa Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Singida

297
0
Share:
Martha Mlata

Mkutano kuu wa uchaguzi CCM mkoa wa Singida umemchagua kwa kishindo Martha Mosses Mlata kuwa Mwenyekiti wa CCM mkoa kuziba nafasi iliyoachwa wazi na Mgana Msindai aliyehamia upinzani.

Mlata ambaye ni mbunge wa viti maalum mkoa wa Singida na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini alipata kura 433 sawa na asilimia 50.08 na kumwacha kwa mbali mpinzani wake wa karibu, Missanga Mohammed Hamisi aliyepata kura 261 sawa na asilimia 30.06.

Mohammed Seif Khatibu

Msimamizi wa uchaguzi maalum wa CCM mkoa, Dk.Mohammed Seif Khatibu, akitoa ufafanuzi juu ya sheria, kanuni na taratibu zitakazofuatwa katika kuchaguzi Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Singida, nafasi iliyoachwa wazi na Mgana Msindai. Kushoto ni Waziri wa Kilimo, Ufugaji na Uvuvi, Mh. Mwigullu Nchemba na kulia ni Mwenyekiti wa muda wa mkutano huo, Mosses Matonya.

Akitangaza matokeo hayo msimamizi wa uchaguzi huo uliofanyikia kwenye ukumbi wa mikutano wa Kanisa la Katoliki mjini hapa, Dk.Mohammed Seif Khatibu,alisema kuwa jumla ya wajumbe 857 wa mkutano huo walipiga kura na kura tano ziliharibika.

Aliwataja wagombe wengine na kura zao kuwa ni Juma Kilimba aliyepata kura 90 sawa na aslimia 10 na Narumba Hanje ambaye alipata kura 69 sawa na aslimia nane.

Mohammed Sief Khatibu

Mwenyekiti wa mkutano Mkuu maalum (CCM) wa uchaguzi mkoa wa Singida, Mosses Matonya, akitoa nasaha zake kwenye mkutano huo uliofanyika mjini Singida. Kushoto ni Waziri wa Kilimo, Ufugaji na Uvuvi, Mh.Mwigullu Nchemba na kulia ni msimamizi wa uchaguzi huo, Dk. Mohammed Seif Khatibu.

Akitoa shukrani zake kwa wapiga kura, Mlata aliahidi kushirikiana na viongozi na wana CCM wote ili pamoja na mambo mengine, mkoa wa Singida uendelee kuwa ngome wa CCM.

“Kwa pamoja tutahakikisha jimbo la Singida mashariki linatoka mikononi mwa upinzani na kulirudisha chini ya mikono ya CCM,” alisema mwenyekiti huyo mteule.

Imeandaliwa na Nathaniel Limu, Singida.

Martha Mlata

Mwenyekiti mteule CCM mkoa wa Singida, Martha Mosses Mlata, akishiriki kupiga kura kuchaguzi wa nafasi ya Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Singida, ambayo yeye alishinda.

Martha Mlata

Mwenyekiti mteule wa CCM mkoa wa Singida, Martha Mosses Mlata, akiwashukuru wana CCM waliomwezesha kushinda kinyang’anyiro hicho na kuwaahidi kushirikaina nao. Kushoto ni Waziri wa Kilimo, Ufugaji na Uvuvi na mbunge wa jimbo la Iramba, Mwigullu Nchemba na kulia ni Katibu CCM mkoa wa Singida, Mary Maziku.

Share:

Leave a reply