Mashabiki wa Urusi watimuliwa kutizama michuano ya EURO 2016

237
0
Share:

Kama ulipata nafasi ya kutazama mchezo wa England na Urusi katika mashindano ya Uefa Euro 2016 yanayofanyika nchini Ufaransa basi utakuwa unaelewa ni jambo gani lilijitokeza baada ya kumalizika kwa mchezo huo.

Katika mchezo huo ambao ulimalizika kwa sare ya goli moja kwa moja, mashabiki wa Urusi na England waligombana huku mikanda ya video ikionyesha kuwa mashabiki wa Urusi ndiyo waliovunja uzio na kuwafata mashabiki wa England.

Kutokana na ugomvi huo, taarifa kutoka nchini Ufaransa zinaeleza kuwa nchi hiyo imeamua kuwarudisha kwao mashabiki 150 wa Urusi kwa kile kinachoelezwa kuwa ni kushiriki vurugu katika mchezo huo.

Mwenedesha mashtaka katika mchezo huo ameeleza kuwa abla ya mchezo huo kulikuwa na mashabiki wengi wa Urusi ambao tayari walikuwa wamejipanga kwenda kufanya vurugu katika mchezo huo.

Kiongozi wa mashabiki wa Urusi, Alexandr Shprygin amesema kuwa kuna mashabiki 29 wa Urusia ambao walipelekwa hadi uwanja wa ndege ili warejee Urusi.

Share:

Leave a reply