“Matumizi ya mbolea ya Urea katika vyakula vya mifugo ni salama”- Serikali

299
0
Share:

Serikali kupitia Wizara ya Kilimo,mifugo na Uvuvi imeelezwa kuwa itaendelea kuendeleza sera yake ya mifugo na unenepeshaji wa mifugo kwani inasaidia na ni nzuri endapo matumizi yake yatafuatwa kwa kiwango kinachotakiwa.

Kauli hiyo imeelezwa leo jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Msaidizi wa uzalishaji wa Wizara hiyo ya mifugo, Bw. Aaron Lugiza alipokuwa kizungumza na wanahabari juu ya Unenepeshaji wa mifugo hapa nchini ambapo kwa kufanya hivyo inasaidia kuongeza ubora wa nyama na thamani ya mifugo kwa kuiwezesha  kuongeza uzito, kufanya nyama kuwa laini na  yenye ladha nzuri.

“Mifugo inayonenepeshwa huandaliwa kwa kupatiwa kinga za magonjwa mbalimbali ikiwemo minyoo na tiba kabla ya kutengwa na kulishwa kwa vyakula vyenye wanga, protini na kupewa maji ya kutosha kwa mahitaji ya unenepeshaji ambapo pia mifugo hiyo uhifadhiwa eneo maalum ilikuepuka kuchungwa iloi nguvu nyingi itumike kuongeza uzito” alieleza Mkurugenzi huyo.

Aidha, Mkurugenzi huyo amebainisha  kuwa, matumizi ya mbolea ya Urea inayotumika katika unenepeshaji ni salama endapo itatumika ipasavyo. Aidha Wizara hiyo imefafanua kuwa Urea inatumika katika nchi nyingi duniani kama chakula cha mifugo hususani ile  inayocheua japo kwa Tanzania inatumika kwa kiwango kidogo sana. (Tazama video hapa chini)

Imeandaliwa na Andrew Chale,modewjiblog

mboleqa ya ureaDaktari mkuu wa mifugo wa Wizara ya Kilimo, Mifugo a Uvuvi, Dk.Sero Luwongo akifafanua jambo juu ya matumizi sahihi ya mbolea ya Urea kwa mifugo hapa nchini ambapo amewatoa hofu watanzania wanaotumia nyama kuwa wapo salama kwani mbolea hiyo ya Urea endapo itazidi kwa kiwango kikubwa kwa mifugo basi mifugo inakufa na wala haiwezi kumfikia mraji. 

ureaMkurugenzi Msaidizi wa uzalishaji wa Wizara ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi, Bw. Aaron Lugiza (wa pili kutoka kulia) akifafanua jambo kwa wanahabari (hawapo pichani). Wengine ni  Afisa wa Wizara hiyo Bi.Suzan Kiyango(wa kwanza kulia). kushoto ni Afisa Habari wa Wizara hiyo ya Kilimo, Bw Bernard Kaari, akifuatiwa na Mganga Mkuu wa mifugo wa Wizara hiyo, Dk. Sero Hassan Luwongo  wakati wa mkutano wao huo na waandishi wa habari mapema leo Februari 19.2016, jijini Dar es Salaam

mifugo 2Baadhi ya wanahabari wakifuatilia mkutano huo  ambapo Mkurugenzi Msaidizi wa uzalishaji wa Wizara ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi, Bw. Aaron Lugiza  akielezea namna ya Wizara yake inavyoshughulikia  sera ya mifugo hapa nchini likiwemosuala la unenepeshaji. (Picha zote na Andrew Chale,modewjiblog)

Share:

Leave a reply