Mauzo ya hisa DSE yashuka kutoka Tsh. 2.5 bilioni hadi 406 milioni

418
0
Share:

Idadi ya Mauzo ya hisa katika Soko la Hisa la Dar es Salaam kuishia wiki ya Februari 10, 2017, yamepungua kutoka Tsh. 2.5 Bilioni hadi  406 Milioni.

Akizungumza na waandshi wa habari, Afisa Masoko na Mauzo wa DSE, Patrick Mususa amesema kushuka kwa mauzo katika soko hilo, kumepelekea Idadi ya hisa zilizouzwa na kununuliwa kupungua kutoka hisa 868,000 hadi hisa 262,000.

Licha ya mauzo kushuka, Mususa amesema ukubwa wa mtaji wa kampuni zilizoorodheshwa katika soko la DSE umeongezeka kwa Shilingi Bilioni 300 kutoka Shilingi Trilioni 18.7 hadi Shilingi Trilioni 19.0 baada ya bei za hisa za makampuni mbali mbali kuongezeka.

Aidha, Mususa amezitaja kampuni tatu zilizoongoza katika mauzo ya hisa kuwa ni

TBL kwa 63.8%,

CRDB  12.4% na

TCC 8.9%.

Pia amesema kiashiria cha kampuni zilizoorodheshwa katika soko DSEI kimeongezeka kwa pointi 35 kutoka pointi 2,146 hadi pointi 2,181 kutokana na kuongezeka kwa bei ya hisa za kampuni mbali mbali zilizopo sokoni ikiwa ni pamoja na ACACIA, DSE, na NMG.

Pamoja na Kiashiria cha kampuni za ndani (TSI) wiki hii pia kimeongezeka kwa pointi 0.6 kutoka pointi 3,380.2 hadi pointi 3,380.8 kutokana na kuongezeka kwa bei ya hisa za kampuni ya DSE.

Wakati Sekta ya viwanda (IA) wiki hii imebaki kwenye kiwango kile kile cha pointi 4,194.

Huku, Sekta ya huduma za kibenki na kifedha (BI) wiki hii imeongezeka kwa pointi 1.5 kutokana na kuongezeka kwa bei ya hisa za DSE kwa asilimia 6 kutoka Shilingi 1,000 hadi Shilingi 1,060 kwa kila hisa.

Share:

Leave a reply