Mauzo ya hisa katika Soko la Hisa la Dar (DSE) yapungua kwa asilimia 23

278
0
Share:

Idadi ya mauzo katika Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE) imepungua kwa asilimia 23% na kufikia sh. 6.4 Bilioni kutoka 8.3 Bilioni wiki iliyopita.

Hali kadhalika,ukubwa wa mtaji wa soko umeshuka kwa wastani wa asilimia 2.1% hadi Trilioni 21.4 kutoka Trilioni 21.9 wiki iliyopita. Pamoja na ukubwa wa mtaji wa makampuni ya ndani umepungua kwa wastani wa asilimia 0.3% hadi Trilioni 8.19 kutoka Trilioni 8.21 wiki iliyopita.

Afisa Miradi na Maeneleo ya Masoko DSE Patrick Mususa amesema licha idadi ya mauzo ya soko kushuka, idadi ya hisa zilizouzwa na kununuliwa imeongezeka mara sita (x6) hadi 11 Milioni kutoka 1.8 Milioni wiki iliyopita.

Aidha, Mususa amezitaja Kampuni tatu zilizoongoza kwa idadi ya hisa zilizouzwa na kununuliwa kuwa ni CRDB kwa asilimia 95.45, ikifuatiwa na TBL kwa 2.18 na DSE kwa1.44%.

Kuhusu viashiria katika sekta za viwanda, buduma za kifedha na kibiashara, amesema sekta ya viwanda imejitokeza wiki hii kupungua kwa wastani wa pointi 17.7 baada ya bei ya hisa za TCC kupungua kwa asilimia 1.7%.

Pamoja na sekta ya Huduma za Kibenki na Kifedha wiki hii imepungua pointi 4.5 baada ya bei ya hisa za DSE kushuka kwa asilimia 6%.

Wakati Sekta ya Huduma za Kibiashara wiki hii imeendelea kubaki kwenye wastani ule ule wa TZS 3,157 sawa na wiki iliyopita.

Share:

Leave a reply