Mawaziri wa Kilimo wa Tanzania Bara na Zanzibar wafanya mkutano wa pamoja na watendaji wa Uvuvi bahari kuu

499
0
Share:

Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi wa Tanzania Bara na  Zanzibar wamekutana na kufanya mkutano na watendaji wa Mamlaka ya Uvuvi wa Bahari Kuu katika mkutano wa pamoja na watendaji wa Mamlaka hiyo,  uliofanyika Fumba, Zanzibar.

DSC_0025Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi Zanzibar Juma Ali Juma akiwakaribisha Mawaziri wanaoshughulikia Uvuvi wa Tanzania Bara na Zanzibar katika Mkutano wa pamoja uliozungumzia mikakati ya kuimarisha Uvuvi wa Bahari Kuu Tanzania uliofanyika Mamlaka ya Usimamizi wa Bahari Kuu Zanzibar iliopo Kijiji cha Fumba, Wilaya ya Magharibi B.

DSC_0043Waziri wa Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi wa Zanzibar Hamad Rashid Mohd akizungumza na watendaji wa Mamlaka ya Uvuvi wa Bahari Kuu katika mkutano wa pamoja uliofanyika Ofisi ya Mamlaka ya Usimamzi wa Bahari Kuu iliyopo Fumba.

DSC_0070Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Uvuvi wa Bahari Kuu Rashid Bakari Hoza akieleza shughuli zinazofanywa na Mamlaka hiyo katika Mkutano uliowashirikisha Mawaziri wanaosimamia masuala ya Uvuvi wa Zanzibar na Tanzania Bara.

DSC_0095 Waziri wa Kilimo,Mifugo na Uvuvi Dkt. Charles Tizeba akisisitiza jambao kwa watendaji wa Mamlaka ya Uvuvi wa Bahari Kuu katika mkutano wa pamoja na watendaji wa Mamlaka hiyo, (kulia) Waziri wa Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi Hamad Rashid Mohd.

Picha na Makame Mshenga/Maelezo Zanzibar.

Share:

Leave a reply