Mbaroni kwa kumwua mtoto wake kwa majini

595
0
Share:

Mwanamke mmoja aliefahamika kwa majina ya Nyamisi Bahati (27 ) mkazi wa kisiwa cha Nyamango kijiji cha Soswa wilayani Sengerema mkoani Mwanza anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za mauaji ya mtoto wake wa kiume, Sakimu Hassan baada ya kumtupia majini katika Ziwa Victoria

Imeelezwa kuwa mtuhumiwa alitoka nyumbani kwa mumewe na kwenda kuwasalimia wazazi wake huku akiwa na mtoto wake baadae alisema amemtupa kwenye Ziwa Victoria.

Wakizungumza kwa masikitiko makubwa baadhi ya wananchi wamesema kuwa kitendo hicho ni cha kinyama hakiwezi kuvumilika huku wakitoa wito kwa mabinti kuwa wavumilivu katika maisha yanapotokea matatizo na sio kuchukua maamuzi ya kikatili 

Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Mwanza, Ahmed Msangi amesema kuwa tayari mtu huyo anashikiliwa na Jeshi la Polisi ambapo uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa ana tatizo la akili na baada ya upelelezi kukamilika atafikishwa mahakamani

Na Veronica Martine, Sengerema

Share:

Leave a reply