Mbunge Bonnah Kaluwa achangisha Milioni 13.7 ununuzi wa eneo la kituo cha yatima

317
0
Share:

Mbunge wa Jimbo la Segerea, Mh. Bonnah Kaluwa ameongoza harambee ya uchangishaji wa fedha za kununua eneo la kituo cha kutoa huduma kwa watoto wanaoishi katika mazingira magumu eneo la Tegeta, harambee iliyoendeshwa na  CVC Deliverance Centre Victorius Church (CVC), chini ya Kiongozi Mkuu Mchungaji Jehu Mkono.

Harambee hiyo ilifanyika katika Kanisa la CVC Deliverance Centre Victorius Tegeta kwa Ndevu, jijini Dar es Salaam, ambapo Mh. Bonnah Kaluwa alikuwa mgeni rasmi na kufanikiwa kukusanya kiasi cha fedha shilingi 13,730,000 ambazo zilipatikana kwa ahadi, michango ya waumini, wageni waalikwa na kufanyika kwa mnada ulionadi vitu mbalimbali.

Katika harambee hiyo Mbunge, Mh. Kaluwa alitoa shilingi milioni mbili yeye pamoja na mumewe huku akiendesha mnada uliotunisha mfuko wa kununua eneo la kituo hicho. Awali akizungumza katika harambee hiyo Mwenyekiti wa umoja wa akinamama wa CVC, Rose Haji Mwalimu alisema harambee hiyo itawezesha kupatikana kwa fedha za kununua eneo la kituo pamoja na upanuzi wa kanisa la CVC eneo la Tegeta mradi unaotarajia kutumia shilingi milioni 40.

Akizungumza wakati wa harambee hiyo, Mh. Kaluwa alimpongeza Kiongozi Mkuu wa CVC Deliverance Centre Victorius Church, Jehu Mkono kwa nia yake ya kuwasaidia watoto wanaoishi katika mazingira magumu kwa kuwajengea nyumba na kumuahidi yeye kama mwakilishi wa serikali atahakikisha analifikisha wazo hilo serikalini ili kuona jinsi gani serikali itamsaidia kutimiza malengo yake.

“Nikupongeze mtumishi kwa jambo ambalo umepanga kulifanya, mimi nitalifikisha wazo lako ili kama serikali tuone jinsi gani tunatoa mchango wetu na kuhakikisha mipango ambayo umeipanga ya kujenga nyumba kwa ajili ya watoto wanaoishi katika mazingira magumu wanapata nyumba ya kuishi,” alisema Mh. Kaluwa.

Mbali na kufundisha neno la Mungu, Kanisa la CVC Deliverance Centre Victorius limekuwa likitoa huduma za kijamii kwa kuhifadhi watoto wanaoishi katika mazingira magumu na watoto yatima ambao kwa namna moja au nyingine wamekuwa wakiishi katika mazingira hatarishi, kituo kikubwa kikiwa Mbeya kilicho na watoto 154.

unnamed-7Kiongozi Mkuu wa CVC Deliverance Centre Victorius, Mchungaji Jehu Mkono (kulia) akishusha maombi kabla ya kuanza kwa harambee hiyo ya uchangishaji wa fedha za ujenzi wa kituo cha kutoa huduma kwa watoto wanaoishi katika mazingira magumu eneo la Tegeta.

unnamed-3Mgeni rasmi Mbunge wa Jimbo la Segerea, Mh. Bonnah Kaluwa (wa pili kulia) akipeana mkono na Mwenyekiti wa umoja wa akinamama Kanisa la CVC Deliverance Centre, Rose Haji Mwalimu (kulia) mara baada kukabidhi risala ya harambee hiyo. Kushoto ni Hoyce Temu, ambaye ni mwanakamati wa harambee hiyo.

unnamed-5

Bishop Fedrick Ndonde ambaye ni rafiki wa karibu wa Kiongozi Mkuu wa CVC Deliverance Centre Victorius Church, Mchungaji Jehu Mkono akizungumza machache kabla ya kumkaribisha Mgeni rasmi Mbunge wa Jimbo la Segerea, Mh. Bonnah Kaluwa (hayupo pichani) kuzungumza na wageni waalikwa pamoja na waumini.

unnamed-1Mgeni rasmi Mbunge wa Jimbo la Segerea, Mh. Bonnah Kaluwa akizungumza katika harambee ya kuchangisha fedha za ujenzi wa kituo cha kutoa huduma kwa watoto wanaoishi katika mazingira magumu eneo la Tegeta, harambee hiyo iliyoendeshwa na Kanisa la CVC Deliverance Centre Victorius, chini ya Kiongozi Mkuu wa kanisa la CVC Deliverance Centre, Mchungaji Jehu Mkono.

unnamed-12Kiongozi Mkuu wa CVC Deliverance Centre Victorius Church, Mchungaji Jehu Mkono (katikati) akitoa ahadi yake mbele ya mgeni rasmi Mbunge wa Jimbo la Segerea, Mh. Bonnah Kaluwa (kulia).

unnamed-13Mgeni rasmi Mbunge wa Jimbo la Segerea, Mh. Bonnah Kaluwa akiendesha mnada wa vitu mbalimbali kwenye harambee hiyo.

img_0694

img_0451Kiongozi Mkuu wa Kanisa la CVC Deliverance Centre, Mchungaji Jehu Mkono (mwenye kipaza sauti) Mwanakati wa Harambee hiyo Hoyce Temu (kulia), Wa pili Kulia ni Bishop Fredrick Ndonde wakifurahi jambo wakati Mh. Bonnah Kaluwa akiendesha mnada. 

unnamed-6Mgeni rasmi Mbunge wa Jimbo la Segerea, Bonnah Kaluwa (kulia) akiteta jambo na Mwanakamati wa harambee ya uchangishaji wa fedha za ujenzi wa kituo cha kutoa huduma kwa watoto wanaoishi katika mazingira magumu, Hoyce Temu (kushoto) kwenye hafla ya chakula cha mchana iliyoenda sambamba na harambe iliyoendeshwa  na CVC Deliverance Centre Victorious Church, Tegeta kwa Ndevu.  

img_0496

Mgeni rasmi Mbunge wa Jimbo la Segerea, Mh. Bonnah Kaluwa akikata keki kuashiria uzinduzi wa harambee hiyo iliyoendeshwa na CVC Deliverance Centre Victorius Church.

unnamed-2

img_0513Mwanakamati wa harambee ya uchangishaji wa fedha za ujenzi wa kituo cha kutoa huduma kwa watoto wanaoishi katika mazingira magumu, Hoyce Temu akiandaa vipande vya keki.

img_0523Mwenyekiti wa umoja wa akinamama CVC Deliverance Centre Victorius Church, Rose Haji Mwalimu akimlisha kipande cha keki mgeni rasmi Mbunge wa Jimbo la Segerea, Mh. Bonnah Kaluwa kwenye harambee hiyo. Kushoto ni Kiongozi Mkuu wa CVC Deliverance Centre Victorius Church, Mchungaji Jehu Mkono na Kulia ni Bishop Fedrick Ndonde ambaye ni rafiki wa karibu wa Kiongozi Mkuu wa kanisa la CVC.

img_0532

Mgeni rasmi Mbunge wa Jimbo la Segerea, Mh. Bonnah Kaluwa akimlisha kipande cha keki Bi. Rose Mwalongo mmoja wa wageni waalikwa kwenye harambee hiyo.

img_0636

Mgeni rasmi Mh. Bonnah Kaluwa na waumini wakisifu na kuabudu kwenye harambee hiyo ambayo ilipambwa na nyimbo za injili kutoka kwa wasanii mbalimbali.

unnamed-8

Baadhi ya wageni waalikwa katika harambee iliyoendeshwa na CVC Deliverance Centre Victorius Church (CVC), chini ya Mchungaji Jehu Mkono wakiwa katika harambee hiyo.

unnamed-10

img_0705

 Kiongozi Mkuu wa CVC Deliverance Centre Victorius Church, Mchungaji Jehu Mkono (kulia) pamoja na rafiki yake Bishop Fedrick Ndonde kwa pamoja wakimkabidhi zawadi Mgeni rasmi Mbunge wa Jimbo la Segerea, Mh. Bonnah Kaluwa (katikati).

img_0708

Mgeni rasmi Mbunge wa Jimbo la Segerea, Mh. Bonnah Kaluwa akifurahia zawadi aliyopewa.

img_0712

Mgeni rasmi Mbunge wa Jimbo la Segerea, Mh. Bonnah Kaluwa kwenye picha ya pamoja na viongozi wa CVC pamoja na wageni waalikwa meza kuu.

img_0717

Mgeni rasmi Mbunge wa Jimbo la Segerea, Mh. Bonnah Kaluwa akiagana na Mshehereshaji wa Harambee hiyi, Edith Temu Max. Kushoto ni

 

 

Share:

Leave a reply