Mbunge Iringa Mjini akamatwa, aachiwa kwa dhamana

404
0
Share:

Mbunge wa Iringa Mjini na Mwenyekiti wa CHADEMA Kanda ya Nyasa Mch. Peter Msigwa aliyekamatwa na polisi jimboni Iringa mjini alipokuwa anaongea na wananchi wa jimbo lake la Iringa Mjini kupitia mkutano wa hadhara jioni ya Septemba 24,ameachiwa kwa dhamana majira ya usiku kwa masharti ya kuripoti kwa Kamanda wa Polisi wa Mkoa huo Jumatatu ya Septemba 25,2017.

Mbunge huyo amewekewa dhamana na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Iringa Mjini Mhe. Alex Kimbe  pamoja na Mwenyekiti wa BAVICHA Wilaya ya Iringa Leonce Marto.

Habari zaidi ya tukio hilo zitawajia kadri tutakapozipata.

Share:

Leave a reply