Mbunge Ridhiwani Kikwete: Chalinze kuwa ya Viwanda

246
0
Share:

Mbunge wa Jimbo la Chalinze lililopo Wilaya ya Bagamoyo Mkoani Pwani, Mh. Ridhiwani Kikwete ameweka wazi kuwa jimbo hilo lipo katika mikakati ya kuwa jimbo la mfano hasa katika uwekezaji wa viwanda ‘Tanzania ya Viwanda’.

Mh. Ridhiwani ameeleza hayo wakati wa tukio la Mgeni rasmi Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mh. William Lukuvi akitoa hati za kurasimisha ardhi kwa mwekezaji wa kiwanda cha uzalishaji wa mabetri kilichopo Chalinze.

Mh. Ridhiwani amebainisha kuwa, mpaka sasa tayari viwanda mbalimbali vimejengwa ndani ya jimbo hilo na vingine vipo mbioni kwani lengo ni kuleta maendeleo na kuunga mkono juhudi za kimaendeleo ikiwemo uchumi wa viwanda.

Mbunge wa Jimbo la Chalinze lililopo Wilaya ya Bagamoyo Mkoani Pwani, Mh. Ridhiwani Kikwete akifurahia jambo na Waziri wa Ardhi  Mh. Lukuvi.

Mgeni rasmi Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mh. William Lukuvi akizungumza katika tukio hilo

Mbunge wa Jimbo la Chalinze lililopo Wilaya ya Bagamoyo Mkoani Pwani, Mh. Ridhiwani Kikwete akizungumza katika tukio hilo 

Share:

Leave a reply