Mbwana Samatta atua nchini kujiandaa na mchezo wa Malawi

230
0
Share:

Nahodha wa Taifa Stars, Mbwana Ally Samatta tayari ametua nchini kuungana na nyota wengine wa Tanzania katika mazoezi yanayofanyika Uwanja wa Boko Veteran, ulioko Boko nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam kujiandaa na mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Malawi utakaofanyika Uwanja wa Uhuru,  Jumamosi Oktoba 7, 2017 kuanzia saa 10.00 jioni.

Samatta amewasili nchini akitokea Ubelgiji alipokuwa akiitumikia klabu anaoichezea ya Genk inayoshiriki Ligi Kuu ya Ubelgiji.

Share:

Leave a reply