Mchakato wa uchaguzi mkuu wa TFF wasimamishwa

822
0
Share:

Mwenyekiti wa Kamati ya uchaguzi mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Revocatus Kuuli ametangaza kusitisha mchakato mzima wa uchaguzi wa TFF hadi hapo utakapotangazwa tena baadae.

Akizungumza na waandishi wa habari, Kuuli amesema sababu ya kusitisha mchakato huo ni kutokuwa na haki kwenye kamati hiyo hivyo yeye kama mwenyekiti ameona ni vyema kusitisha hadi hapo hatua zingine zitakapochukuliwa.

“Siwezi Kuendelea na machakato usiokuwa na haki, watu wanawakata wagombea bila sababu za Msingi! Uonevu Huo Nimeshindwa Kuuvumilia, nimeona kwakua nina mamlaka yakusitisha mchakato basi nikamwandikia Katibu mkuu barua na yeye akakaa kikao na Sekretarieti,

“Wamekubali ombi hilo. Hivyo kuanzia sasa mchakato wa uchaguzi umesitishwa mpaka pale utakapotangazwa tena,” amesema Rovacatus Kauli wakati akitangaza kusitishwa mchakato wa uchaguzi wa TFF.

Share:

Leave a reply