Mchezaji wa Marekani avunjiwa mkataba kwa vitendo vya kihalifu

216
0
Share:

Mchezaji wa timu ya San Francisco 49ers ya nchini Marekani, Bruce Miller amekatishiwa mkataba wake na klabu hiyo kufuatiwa kukamatwa kwa madai ya kuhusika na vitendo vya kiharifu.

Ripoti ambayo imetolewa na klabu hiyo imeleza kuwa imevunja mkataba na mchezaji huyo mwenye miaka 29 na hivyo kuanzia sasa hataitumikia tena.

“San Francisco 49ers inatangaza wamemwachia beki wa kulia Bruce Miller,” ilisema taarifa hiyo.

Miller alikamatwa kwa kuhusika kumshambulia mzee wa miaka 70 na mjukuu wake wa kiume ambao baadae walipelekwa hospitali kwa ajili ya kupatiwa matibabu.

Tukio lilitokea jumapili usiku katika hoteli iliopo San Francisco na inasemekana kabla ya kutokea kwa shambulio hilo kulikuwa na mabishano ambayo yalisababisha kutokea kwa tukio hilo la shambulizi.

Share:

Leave a reply