“Mchezo wa Prisons kwetu ni kama fainali”- Niyonzima

654
0
Share:

Kuelekea mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kati ya mabingwa watetezi wa kombe hilo Yanga na Prisons ya Mbeya, nahodha msaidizi wa klabu hiyo amezungumza kuhusu mchezo huo.

Akizungumza na Global TV, Haruna Niyonzima amesema mchezo huo utakuwa utakuwa muhimu kwa timu yake kushinda ili kujiweka katika mazingira mazuri ya kutetea kombe la VPL.

“Mara nyingi siangalii historia, mara nyingi naangalia wakati uliopo, haijarishi tumewashinda mara ngapi au tumewafunga goli ngapi, kila mchezo una picha yake sisi kitu kikubwa hatutakiwi kupoteza mchezo

“Mchezo wa kesho kwetu ni kama fainali. Ni mchezo ambao utarudisha morali, utakuwa mchezo mgumu na tunatakiwa kuwa pamoja ili kupata pointi tatu,” amesema Niyonzima.

Aidha amezungumzia mchezo wa nusu fainali ya kombe la FA ambao walifungwa na timu ya Mbao na kusema kuwa, “Mtu yoyote ambaye aliona mechi hawezi kusema jambo lolote, Mwenyezi Mungu alikuwa hajatupangia kushinda ile mechi, wachezaji tulijitahidi lakini ilishindikana, tulikuwa na malengo ya kushinda FA lakini mambo mengine unaweza kupanga na yasifanikiwe.”

Share:

Leave a reply