MeTL Group yakabidhi mradi wa utunzaji mazingira kwa S/M Gilman Rutihinda

349
0
Share:

Kampuni ya Mohammed Enterprises Tanzania Limited (MeTL Group) kwa kushirikiana na Taasisi isiyo ya kiserikali ya Roots & Shoots wamekabidhi mradi wa utunzaji mazingira kwa shule ya msingi Gilman Rutihinda.

Mradi wa Utunzaji wa Mazingira ulianzishwa Agosti, 17 ukiwa ni mpango endelevu unaolenga kutoa elimu kwa jamii kuhusiana na njia sahihi za kutunza mazingira na kuboresha miundombinu asilia

Aidha ushirikiano baina ya  Kampuni ya Mohammed Enterprises na Taasisi ya mazingira ya ‘Roots & Shoots’ umebadilisha mazingira na muonekano wa shule ya msingi Gilman Rutihinda kwa kuwezesha kutengeneza vitalu vya maboksi (Box Garden) na viriba vya miti vipatavyo 2311.

img-20161007-wa0059Mmoja wa wafanyakazi wa MeTL akiwaekeleza wanafunzi wa shule ya msingi Gilman Rutihinda namna ya kuotesha vitalu hivyo.

img-20161007-wa0049Mmoja wa wanafunzi wa shule ya msingi Gilman Rutihinda akiendelea na zoezi la kupanda vitalu hivyo.

img-20161007-wa0057Mmoja wa wafanyakazi wa MeTL akishiriki zoezi hilo na wanafunzi wa shule ya msingi Gilman Rutihinda kuotesha vitalu vya miti.

img-20161007-wa0063Zoezi la kuotesha vitalu likiendelea kwa kushirikiana na mmoja wa wafanyakazi wa MeTL.

img-20161007-wa0068Picha ya pamoja ya wafanyakazi wa MeTL, wadau wa Taasisi ya mazingira ya ‘Roots & Shoots’ pamoja na baadhi ya wanafunzi wa shule ya msingi Gilman Rutihinda.

img-20161007-wa0045Sehemu ya muonekano wa hivi sasa wa vitalu vya maboksi (Box Garden) na viriba vya miti vipatavyo 2311 katika shule ya msingi Gilman Rutihinda.

Share:

Leave a reply