Meya Dar awataka Watanzania wasiwe watumwa wa lugha, ampongeza JPM

629
0
Share:

Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita amewataka watanzania kuienzi lugha ya Kiswahili na kuifanya kama chanzo cha ajira hususani katika kipindi hiki ambacho imeundwa Tume ya Kiswahili ya Afrika Mashariki na kwamba itahitaji wataalamu wengi wa Kiswahili.

Mwita ameyasema hayo Jumapili ya Desemba 18,2016 wakati wa utolewaji tuzo ya mshindi wa Tuzo ya Ushairi ya Mstahiki Meya wa Dar es Salaam.

“Tumeamua kuwa watumwa wa lugha baadhi ya sehemu muhimu tunatumia kiingereza,” amesema na kuongeza.

“Tuienzi lugha yetu adhimu ya kiswahili, tukiacha ipotee katika vizazi vijavyo tutavunja heshima ya wazee wetu walioianzisha.”

Nchi za Uganda, Rwanda, Malawi, Msumbiji sasa wanajifunza lugha ya lugha ya kiswahili kutokana na kutambua umuhimu wake, tukishangaa lugha hiyo itapotea nchini na kukua kwa wenzetu,” amesema.

Aliyekuwa Waziri wa zamani wa Habari, Utamaduni na Michezo Zanzibar, Seif Khatib amewahasa watanzania kuitumia lugha hiyo kama bidhaa ya kujipatia kipato kutokana kwamba nchi nyingi mashughuli duniani zinaonyesha nia ya kujifunza kiswahili.

“Hamuwezi mkaijua thamani ya kiswahili hadi pale kitakapopotea, lugha hii ni mfadhili mkubwa wa watanzania na ni bihaa muhimu ingawa hatuioni,

“Nampongeza Rais Magufuli kwa kutumia kiswahili katika sherehe, hotuba na dhifa za kiserikali hata kama wageni si waswahili,” alisema.

Share:

Leave a reply