Meya Mwita afuturisha wakazi wa Dar es Salaam

316
0
Share:

Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita jana Juni 16, 2017 alifuturisha wakazi zaidi ya mia kutoka sehemu mbambali za jiji hilo, katika viwanja vya Kareem Jee.

Akizungumza baada ya hafla hiyo kumalizika, Meya Mwita alisema lengo la kuifanya hafla hilo ni kuungana na waumini wa Kiislamu wa jiji hilo ambao wako katika mwezi mtakatifu wa mfungo wa Ramadhan.

“Nimefuturisha leo, na si mara ya kwanza kila mara nimekuwa nikifanya hivyo, lengo ni kuwakutanisha wakazi wa Dar es Salaam ambao wametoka sehemu mbalimbali,” amesema

 Naye Mbunge wa Temeke, Abdallah Mtolea alimpongeza Meya Mwita kwa kuandaa hafla hiyo, na kusema kuwa imesaidia kuwakutanisha na wananchi wao ambao si rahisi kukutana nao kutokana na shughuli zao.

“Nimefurahi, nimejumuika na masheikh wakubwa pamoja na wananchi ambao sio rahisi kwa sisi viongozi kukutana nao, lakini kupitia hafla hii tumepata fursa ya kukutana nao,” amesema.

Naye Sheikh wa Wilaya ya Ilala, Adam Mwinyipingu alimpongeza Meya Mwita kwa kuandaa hafla hiyo. 

kwa upande wa wananchi waliohudhuria katika hafla hiyo walimshukuru Mwita, na kumtaka aendelee kuwa na desturi hiyo ya kuwakutanisha wakazi wa jiji lake.

 Na Regina Mkonde  

Share:

Leave a reply