Mfanyabiashara wa Utalii Arusha atoa misaada ya kijamii hospitali mkoa wa Arusha

262
0
Share:
Violet Mfuko

Katika kuelekea maadhimisho ya kilele cha siku ya wanawake duniani Machi 8 baadhi ya wanawake jijini Arusha wanaadhimisha siku hiyo kwa matukio mbalimbali ambapo mwanamke mjasiriamali wa jijini humo Violet Mfuko amejitolea kujenga sehemu ya kusubiria na kufanyia ibada katika mochwari ya hospitali ya Mt. Meru mkoa wa Arusha  pamoja na mashimo nane ya vyoo katika sehemu hiyo.

Akiwa ameongozana na wakina mama wengine walianzia kutoa msaada wa vitu mbalimbali katika wodi ya wanawake na watoto ambapo Violet  anasema baada ya kutembelea sehemu ya mochwari katika hospitali  hiyo aligundua changamoto hiyo ambayo ilimgusa na kuamua kujitolea kuanza ujenzi wa jengo hilo kuanzia jumatatu Machi 7 ambalo litagharimu kiasi cha shilingi milioni 50.

Alisema ameamua kujikita katika kusaidia jamii badala ya kutumia fedha zake katika mambo ambayo hayana faida kwa jamii na kusisitiza kuwa baada ya kupewa ramani na uongozi wa hospitali ataanza ujenzi jumatatu Machi 7 mwaka huu.

1 (1)

Mkurugenzi wa kampuni ya utalii ya Viola, Violet  Mfuko akizima mshumaa alipokuwa akiazimisha siku yake ya kuzaliwa iliyofanyikia katika hospitali ya Mt. Meru jijini Arusha jana.

Alisema baada ya kujionea adha wanayoipata wafiwa kukosa sehemu ya kusubiria miili ya marehemu na vyoo vinavyotumika kuwa ndani ya mochwari aliguswa na suala hilo na kuamua kujenga vyoo na sehemu hiyo.

“Tayari nimeshapokea ramani nitaanza ujenzi jumatatu nawaomba wana Arusha mnipe ushirikiano tuweze kumsaidia Rais Magufuli yeye alianza na Muhimbili sisi tumeamua kumsaidia hospitali yetu ya mkoa”alisema Violet.

Violet ambaye ni Mkurugenzi wa kampuni ya Viola Car Hire yenye makao makuu yake jijini Arusha anatumia siku yake ya kuzaliwa kutoa msaada katika hospitali hiyo na kutoa wito kwa wakazi wa mji wa Arusha kuanza kuisadia serikali kuboresha sekta ya afya kwa kuwa sekta hiyo ina changamoto nyingi.

“Mimi nikiwa ni mwanamke ninajua changamoto nyingi zinazotukabili kina mama na watoto ambapo naamini ukimsaidia mama na mtoto umegusa jamii nzima”alisema Violet

Mkurugenzi wa Kampuni ya Utalii ya Viola,Violet  Mfuko akikata keki alipokuwa akisherekea siku yake ya kuzaliwa iliyofanyika katika hospitali ya Mt.Meru iliyoko jijini Arusha jana.

Hata hivyo baadhi ya wajasiriamali wengine wa jijini humo wanaunga mkono jitihada za mwanamama huyo  ambapo Daktari Edmund Matafu anajitolea mashine mbili za hewa safi kwa ajili ya kusaidia watoto wanaozaliwa kabla ya muda yaani njiti.

Mganga mfawidhi wa hospitali ya mkoa ya Mount Meru Jackline Uriyo amemshukuru Violet na Dakta Matafu kwa  msaada wao ambao amesema umefika  wakati mwafaka.

“Kwa niaba ya uongozi wa hospitali ya Mount Meru tunatoa shukrani za dhati kwa Viola na dakta Matafu tunawaomba waendelee na moyo huo lakini tunatoa wito kwa watu wengine wenye mapenzi mema kuisaidia hospitali ya mkoa kwani inalabiliw na changamoto nyingi”alisema Uriyo

Mbali na msaada huo Viola pia ametoa msaada wa vitu mbalimbali vikiwemo mashuka mia mbili, sabuni, mchele, juisi soda na mablanketi vyote vikiwa na thamani ya shilingi milioni kumi.

Mkurugenzi wa kampuni ya Utalii ya Viola, Violet Mfuko akimlisha keki Mkurugenzi mwenzake, ambae ni (mume wake) ndugu Kim Godwin Fute, alipokuwa akiazimisha siku yake ya kuzaliwa iliyofanyika katika hospitali ya Mt.Meru iliyoko jijini Arusha jana.

Mkurugenzi wa kampuni ya utalii ya Viola,Violet Mfuko akimkabidhi shuka Mganga Mkuu Mfawidhi wa hospitali ya Mt. Meru Dr. Jackline Urio alipokuwa akiadhimisha siku yake ya kuzaliwa jana.

1 (7)

Mkurugenzi wa Kampuni ya Utalii ya Viola, Violet Mfuko akimuombea mgonjwa Frida Shayo alipotembelea hospitali ya Mt.Meru alipokuwa akiadhimisha siku yake ya kuzaliwa jana.

1 (8)

Mkurugenzi Viola Mfuko anamlisha keki Habibya Fadhili alipotembelea hospital ya Mt.Meru alipokuwa akiadhimisha siku yake ya kuzaliwa jana.

Share:

Leave a reply