Mh.Mwigulu Nchemba afanya ziara Kilombero na Iringa kupanua wigo wa uzalishaji wa mbegu na utafiti wa mazao

366
0
Share:

Waziri wa Kilimo,Mifugo na Uvuvi Mh.Mwigulu Nchemba  amewahakikishia wananchi kuwa serikali ya awamu ya tano ya Rais John Magufuli imejipanga kutetea haki za wananchi na itamuwajibisha yeyote anayehujumu kilimo na ustawi wa Taifa.

Waziri Nchemba amesema hayo katika ziara yake anayofanya katika mikoa ya Morogoro na Iringa katika maeneo mbalimbali ya wakulima na mashamba ya wananchi na wadau wengine katika sekta hiyo.

Wizara inajipanga kuandaa mfumo mzuri wa kuhakikisha kila mwananchi anafikiwa kupata pembejeo kwa wakati na upatikanaji wake uwe rahisi.

Lakini,Mwigulu Nchemba pia amewasihi sana wawekezaji kwenye mashamba n.kuheshimu taratibu za uwekezaji,ili kuondoa mahusiano mabaya kati ya muwekezaji na wananchi.Mwisho,Mh.Mwigulu Nchemba anaendelea na ziara yake ya kukagua vituo vya utafiti,Mashamba ya mbeguna,Mifugo na uvuvi katika Mkoa wa mbeya kuanzia tar.5/03/2016.

Nchemba3Waziri wa Kilimo,Mifugo na Uvuvi Mh.Mwigulu Nchemba akiteta jambo na Mbunge wa Mlimba Bi.suzan Kiwanga(CHADEMA) mapema hii leo wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika kijiji cha Mgeta-Mlimba.Pichana Festo Sanga

nchemba72Waziri wa Kilimo akipewa maelezo kuhusu uhudumiaji wa mashamba ya Mahindi kuanzia uaandaji wa shamba, mbegu,mbolea na majira ya kupanda mahindi.Wakati wa ziara hiyo,Mwigulu Nchemba mwenye dhamana ya kilimo ameendelea kusisitiza kuwa kuna haja kama Taifa kuachana na kilimo cha jembe la mkono,lakini matumizi ya mbegu bora na mbolea bora ni muhimu yazingatiwe.

nvMh.Mwigulu akiangalia sehemu ya mpunga uliohalibiwa kwa kile kinachodhaniwa ni sumu iliyotokana na Umwagiliaji wa sumu aina ya Glyphosate iliyokuwa inatumiwa na wamiliki wa KPL kuchoma nyasi kwenye mashamba yao,Katika kikao cha pamoja cha wananchi,Uongozi wa serikali na uongozi wa KPL(Kilombero Plantation Limited),Mwigulu Nchemba amepokea hatua za awali za wataalamu na watafiti wa serikali waliobobea kubaini chanzo cha mimea kuharibika kwa kiasi kikubwa hivi,Wataalam hao wamemhakikishia Mh.Mwigulu Nchemba kuwa watatoa ripoti yao kamili ndani ya muda wa siku 21 ili kubaini aliyesababisha mimea ya mpunga kuungua.

Nchemba1Moja ya mashine za Umwagiliaji kwenye mashamba ya Mpunga ya KPL(Kilombero Plantation Limited) ikiwa tayari kwa kuanza kazi ya kumwagilia maji kwenye shamba hili la mpunga.

NchembaMoja ya trekta la kisasa la muwekezaji wa “Ruaha Farm” ambalo linatumika kupanda mbegu,kuvuna na mwagilia dawa ya mimea.

Share:

Leave a reply