Mhandisi Kamwele atembelea miradi ya DAWASA ya uboreshaji miundombinu ya maji

222
0
Share:

Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Isack Kamwele, ameanza ziara ya siku mbili ya kukagua baadhi ya miradi inayosimamiwa na Mamlaka ya Maji  Safi na Maji Taka, (DAWASA), jijini Dar es Salaam, Desemba 5, 2017.

Katika siku yake ya kwanza ya ziara hiyo, Waziri alitembelea Mradi wa Uboreshaji Mfumo wa Usambazaji maji ambapo kazi zinazofanyika chini ya mradi huo ni pamoja na ujenzi wa matenki tisa (9) ya kuhifadhi  a kusambaza maji  yenye ukubwa wa kuhifadhi lita milioni 3.0 hadi

milioni 6.0, lakini pia ujenzi wa vituo vine(4) vya kusukuma maji, ununuzi na ufungaji wa pampu kubwa 16 za kusukuma maji, ununuzi wa transfoma  na ufungaji njia za umeme wa msongo mkubwa, ununuzi na ulazaji wa mabomba makubwa ya ugawaji maji na ulazaji wa mabomba ya usambazaji maji yatakayokuwa na urefu wa kilomita 477.

Mradi huu utanufaisha maeneo ya Salasala, Bunju, Wazo, Makongo, Changanyikeni , Bagamoyo, Mpiji, Zinga, Kiromo,Kitopeni, Ukuni, Kerege, Buma, Mataya na ukanda maalum wa EPZA ambayo ni maeneo yanayohudumiwa na mtambo wa maji wa Ruvu Chini.

Aidha maeneo mengine yatakayonufaika na mradi huu ni yale yaliyopo kati ya Mbezi Louis, Kiluvya, Kibamba,Mbezi, Makuzi, Makabe, Malamba mawili na Msigani. Maeneo yote haya hupata huduma kutoka Mtambo wa Ruvu Juu ambao ulizinduliwa na Mhe. Rais wa Jamhurim ya Muungani wa Tanzania Juni 21, 2017.

NA K-VIS BLOG/Khalfan Said

 Mhandisi Kamwele, mtendaji Mkuu wa DAWASA, Mhandisi Romanus Mwang’ingo wakimsikiliza Mkandarasi, wapili kulia), na Mtendaji Mkuu wa DAWASCO, Mhandisi Cyprian Luhemeja wakitembelea eneo la ujenzi wa trenki la kuhifandia maji, Mabwepande nje kidogo ya jijji
 Mhandisi Kamwele akizungumza katika moja ya maeneo aliyotembelea
 Mtendaji Mkuu wa DAWASA, Mhandisi Romanus Mwang’ingo wakimsikiliza Mkandarasi, akimsikiliza Mkandarasi anayejenga matenki ya kuhifadhia maji kwenye mradi mjuybwa wa kuimarisha miundombinu unaosimamiwa na DAWASA
 Mhe. Waziri Mhandisi Kamwele, (wapili kushoto), Mtendaji Mkuu wa DAWASA, Mhandisi Romanus Mwang’ingo wakimsikiliza Mkandarasi, Mhandisi
P.G. Rajani wa kampuni ya WAPCOS limited ya india
 Mhe. Waziri Kamwele, (kushoto), akiwa na Mhandisi Romanus Mwang’ingo, wakipatiwa maelezo ya utekelezaji wa mradi ya ujenzi wa tenki la maji eneo la Salasala kutoka kwa mkandarasi, Mhandisi P.G. Rajani wa kampuni ya WAPCOS limited ya india
 Mhe. Waziri Kamwele, (kushoto), akifafanua jambo, wakati akipatiwa maelezo na Mkandarasi kutoka kampunin ya India ya WAPCOS, Mhandisi P.G. Rajani
Waziri Mhandisi Isack Kamwele, (kushoto), akiwa na Mtendaji Mkuu wa DAWASA, Mhandisi Romanus (katikati) na Mtdnaji Mkuu wa DAWASCO, Mhandisi Cyprian Luhemeja.
Share:

Leave a reply