Mhanga aua askari 41 Yemen

312
0
Share:

SHAMBULIO la kujitoa mhanga lililofanyika katika mji wa Kusini wa Yemen wa Aden limeua askari 41 na kujeruhi wengine wawili.

Shambulio hilo limefanyika katika kambi ya jeshi ya Al Solban iliyopo wilaya ya Khor Maksar, wakati askari wamesimama foleni kupokea mshahara.

Imeelezwa kuwa mhanga huyo aliingia katika kambi hiyo akiwa amevalia mavazi ya askari.

Aden mji mkuu wa sasa wa serikali inayotambuliwa na Umoja wa Mataifa na Saudi Arabia imekuwa katika ulinzi mkali dhidi ya majaribio ya waasi wa Houthi ambao wanashikilia mji mkuu wa Sanaa.

Shambulio hilo limefanyika wiki moja toka lifanyike la waasi wa IS ambapo askari 50 waliuawa.

Al Qaeda na  Islamic State kwa miaka miwili wamekuwa wakifanya mashambulio maeneo ya Kusini ambayo hayana utawala wa kisheria lakini yanayodhibitiwa na serikali.

Share:

Leave a reply