Mhubiri wa Marekani apongeza jitihada za Serikali kupambana na dawa za kulevya

826
0
Share:

Raia wa Marekani mhubiri wa dhehebu la kikristo, Keneth Paul, ameipongeza serikali ya awamu ya tano kwa hatua yake ya kuanzisha vita dhidi ya mapambano ya madawa ya kulevya nchini,ili kuokoa wananchi wake kuathirika na madawa hayo.

Aidha,alisema vita hiyo ishiishie kwenye miji na majiji iende hadi ngazi ya vijiji kwa madai huko ndiko baadhi ya madawa yanalimwa.

Mhubiri Paul ametoa pongezi hizo juzi muda mfupi baada ya basi la mgamba alililokuwa akisafiria kutoka Arusha kwenda  Mwanza,kupekuliwa na jeshi la polisi kwa kutumia mbwa.

Alisema yeye binafsi ni shuhuda mzuri wa athari za madawa ya kulevya,kwa madai ametumia madawa ya kulevya ya aina mbalimbali kwa kipindi cha miaka 12.

“Madawa ya kulevya hayana faida yo yote kwa maisha ya binadamu na hasa kwa vijana.Mtumiaji wa madawa hayo hawezi kuwa na maendeleo ya aina yo yote.Atabaki kuwa tegemezi maisha yake yote.Mungu aisaidie Tanzania iondokane na madawa ya akulevya,” alisema mhubiri huyo.

Kuhusu maisha yake,alisema baada ya kubaini watumiaji wenzake wakiathirika na madawa ya kulevya na hawawezi kujiletea maendeleo,aliamua kuachana nayo na kuweka dhamira ya kumutumikia Mungu sehemu mbalimbali za dunia.

Na Nathaniel Limu, Singida

Share:

Leave a reply